Mwakyembe, Mkola Washinda kwa Knock Out Usiku wa Kisasi, Chokoraa Ang’ara

 

Bondia wa ngumi za kulipwa Emmanuel Mwakyembe amefanikiwa kumchapa Hamisi Morinyo kwa TKO ya raundi sita katika pambano la usiku wa kisasi lililopigwa kwa raundi nane na kumaliza utata wa Mburahati na Manzese uliokuwepo muda mrefu.

 

Katika pambano hilo ambalo limepigwa kwenye jana Usiku kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa ambapo mabondia hao walicheza pambano kuu kwa raundi nane lakini lilishia raundi ya sita kwa TKO kufuatia mwamuzi kumaliza kwa kumuokoa Morinyo ambaye alikuwa amechapika vilivyo.

 

Lakini Said Mkola amefanikiwa kumchapa kwa TKO ya raundi ya pili Jackson Malinyingi katika pambano la raundi nane huku Mohamedi Omari akifanikiwa kuweka rekodi ya kulipa kisasi kwa kumchapa kwa pointi Frank Yared.

 

 

 

Tampela Mahurusi ambaye ameshinda kwa pointi dhidi ya Abubakar Kihiyo katika pambano la raundi sita lakini Kihiyo akiwa amechakazwa vizuri uso wake.

 

James Kibazange na Ramadhan Kumbele pambano lao limemalizika kwa sare lakini Kibazange hakuwa tayari kuyakubali matokeo hayo kutokana kudai alistahili ushindi wa kumchapa mpinzani wake aliyeonekana kupendelewa.

Ally Ngwando ambaye ni bingwa wa PST ameendeleza ubabe wake kwa kumchapa kwa TKO ya raundi ya pili Ramadhan Msham lakini mtemi wa Morogoro, Joseph Mchapeni amejikuta akichapwa kwa KO ya raundi ya dhidi ya Abuu Malume.

 

 

Ezra Paul kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ, ameshinda kwa pointi pambano lake kwa kwanza la ngumi za kulipwa dhidi ya Shabaan Mtengela ambalo limepigwa kwa raundi nne.

 

Ally Kilongola amepoteza mbele ya Hemed Rashid na Saleh Kasim amechapa bondia kutoka Zanzibar Ally Mkojani katika pambano la ubingwa wa Taifa wa TPBRC.

 

Wengine walioshinda ni Haidari Abdallah ambaye amechapa kwa TKO Makame Juma, Omari Mpemba akimchapa kwa KO John Widambwe, Abdul Ubaya akishinda kwa KO dhidi ya Shafii Idrisa na Mrisho Mzezele akimchapa kwa pointi Omary Manzi.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment