The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mwalimu Ajichinja Ili Afe Kisa Ugumu wa Maisha

MWALIMU wa Shule ya Msingi Rung’abure iliyopo Serengeti mkoani Mara, Godfrey Tarimo,  amejikata na chupa eneo lake la shingo katika jaribio la kutaka kujiua kwa kile alichosema ni kuzidiwa na ugumu wa maisha na mahusiano mabaya na jirani zake.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere, Wilaya ya Serengeti, Dkt. Tanu Warioba,  amethibitisha kumpokea mwalimu huyo usiku wa Julai 3, 2019,  akiwa ameletwa kwa msaada wa walimu wenzake.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu,  amesema hatua kali za kinidhamu na sheria zitachukuliwa kwa mwalimu huyo ikiwezakana hata kufukuzwa kazi.

Comments are closed.