The House of Favourite Newspapers

Mwalimu akitongoza ‘kiseregenti’ cha miaka 12, chamzalisha mtoto

0

madam (1)Mwalimu Michelle Sulzicki (28) anayedaiwa kufanya ngono na mwanafunzi wa miaka 12 hadi kupata ujauzito.
madam (3)Mahakama ikimsomea mashtaka Mwalimu Michelle Sulzicki (hayupo pichani).madam (2)

MWALIMU wa kike nchini Marekani,  Michelle Sulzicki (28) anadaiwa alifanya ngono zaidi ya mara 20 na mvulana mdogo mwenye umri wa miaka 12, ambapo mvulana huyo hivi sasa anahofu kwamba mtoto aliyezaa mwalimu huyo ambaye sasa ana umri wa miezi mitano ni wa kwake.

Katika kufanya uchunguzi, polisi wamesema kwamba mwalimu huyo aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Msingi ya Stratford, Jimbo la Connecticut, alifanya ngono kwa siri na mvulana huyo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

Vilevile, katika ripoti iliyotolewa na vyombo vya habari, mvulana huyo aliwaambia walimu wake kwamba yeye na Michelle Sulzicki walifanya ngono kiasi cha mara 20, ikiwa ni pamoja na ngono ya kutumia midomo, na ngono ya kinyume na maumbile.

Mvulana huyo anatarajiwa kufanyiwa kipimo cha kugundua iwapo ndiye baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na mwalimu huyo.  Hilo limekuwa ni lazima kwa vile polisi walisema wawili hao walifanya ngono bila kutumia kinga (kondom).

Kwa mujibu wa gazeti la Daily News, mwanafunzi huyo alifichua udhalilishaji huo  aliofanyiwa kwa kuwaambia walimu wake akiwa kwenye shule yake mpya baada ya kuondoka katika Shule ya Msingi ya Stratford,  huko Connecticut.

Mwanafunzi huyo aliwaambia wachunguzi wa tukio hilo kwamba Sulzicki, 28, alikuwa akimvutia kwa kumpa zawadi mbalimbali, lakini aliripoti tukio hilo la kudhalilishwa akiwa anahofia kwamba huenda alimpa ujauzito, liliandika gazeti la Connecticut Post.

Wakati akijisalimisha kwa polisi jana, mwalimu huyo, alikana madai hayo dhidi yake lakini baadaye alikiri kufanya ngono na mvulana huyo mara moja tu.

Sulzicki anashitakiwa kwa makosa mawili ya shambulizi la ngono na kufanya ngono na mtoto mdogo.

Leave A Reply