The House of Favourite Newspapers

Mwalimu Mtuhumiwa Kumpa Mimba Denti Aachiwa Tena

MAHAKAMA ya Hakimu Kazi Mkoa wa Kigoma, imemwachilia huru kwa mara nyingine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Jason Rwekaza, aliyeachiliwa huru kwa mara ya kwanza Septemba 16 na kukamatwa tena Septemba 19 mwaka huu kwa tuhuma tatu za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wake.

Rwekaza ameachiwa huru baada ya upande wa serikali kusema haina nia ya kuendelea na shtaka hilo.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Elia Baha,  anasema amemwachia huru chini ya kifungu cha 91 kifungu kidogo cha 1 cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Comments are closed.