The House of Favourite Newspapers

MWALIMU ATIWA MBARONI KISA KUZAA NA MADENTI WAWILI

0
MWALIMU ATIWA MBARONI
Mwalimu Ibrahim.

 

DAR ES SALAAM: Mwalimu wa kituo kimoja cha elimu mbadala ya sekondari (QT) kilichopo Mabibo jijini hapa, aliyefahamika kwa jina moja la Ibrahim, hivi karibuni alitaitiwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Urafiki akidaiwa kuwazalisha wanafunzi wake wawili kisha kuwatelekeza.

 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwalimu huyo alikuwa akiwafundisha wanafunzi hao waliotambulishwa kwa jina mojamoja, Jovita na Agnes masomo ya jioni kisha akatumia nafasi hiyo kuwarubuni na mwisho kuwazalisha.

 

“Huyu mwalimu alikuwa akiwafundisha wanafunzi hao lakini cha ajabu kawatundika mimba wote wawili kisha kawatelekeza.

 

“Wanafunzi hao walikuwa wanasoma kituo kimoja cha QT lakini walikuwa hawajuani,” kilisema chanzo hicho. Gazeti la Amani lilinasa picha za mshikemshike wa wanafunzi hao, polisi na mwalimu huyo wakati akifikishwa kituo cha polisi kwa ajili ya maelezo zaidi.

 

MWANAFUNZI WA KWANZA

Kwa upande wa Agnes alisema: “Nilikuwa nasoma kwenye kituo ambacho mwalimu Ibrahim alikuwa anafundisha na nilienda pale kwa ajili ya kupata elimu ya sekondari kwa miaka miwili (QT) lakini mwaka juzi, nilipokuwa kidato cha pili, alinirubuni na kunipa mimba.

 

“Waliokuwa wananisomesha walichukia sana na kunikatisha masomo. Nilimtafuta mwalimu na kumueleza, akadai atanipangishia chumba.

 

ATELEKEZWA NA MTOTO

“Mwanzoni alikuwa akinipa matumizi lakini ghafla akasitisha kuwa ananipa huduma, nikajikuta naishi maisha magumu sana.”

 

MSIKIE MWANAFUNZI WA PILI

“Na mimi ilikuwa ni kama ambayo mwenzangu amesimulia, sasa sikujua kama alikuwa anatembea na sisi sote kwa kipindi kimoja.

 

“Hata mimi alinipangishia chumba na alikuwa akinipa matumizi ya kiaina lakini baadaye akanitelekeza. Nikaanza kuhangaika na mtoto peke yangu,” alisema Jovita.

 

DARASA MOJA HAWAKUGUNDUANA

“Mimi na Agnes tulikuwa tunasoma darasa moja lakini hatukuwa tunajuana kama mwalimu anatuchanganya wote anapenda kukaa na kufanyia kazi.

 

MWALIMU ANASWA Baada ya kumsaka kwa muda, hatimaye Jumatatu iliyopita tulifanikiwa kumnasa akiwa Mabibo-Makutano na kufikishwa katika kituo hicho cha polisi cha Mpakani ambapo alihojiwa na kisha kuhamishiwa Kituo cha Urafiki.

 

SHANGAZI ASIMULIA

Akizungumza na gazeti hili, shangazi wa Jovita aliyejitambulisha kwa jina moja la Anna, ambaye ndiye aliyekuwa akimsomesha, alisema alisikitishwa sana na kitendo cha mwalimu kumrubuni binti yake na kumzalisha. “Ukweli roho iliniuma sana baada ya kusikia binti niliyemlea na kuamua kumsomesha kwa gharama, anapewa mimba tena na mwalimu wake.

 

Kumbe hakuwa binti yangu peke yake, yupo na mwingine na wote amewapangishia na kuwatelekeza,” alisema shangazi huyo. Kufuatia sakata hilo, Gazeti la Amani, lilimtafuta Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Mulilo Jumanne, ambaye alisema taarifa hiyo bado haijafika mezani kwake na kuahidi kufuatilia.
kwa wakati mmoja.

 

WAGUNDUA ANA MKE MWINGINE

“Baadaye katika kupeleleza ndipo tukagundua kuwa kumbe mwalimu alikuwa anaturubuni na kutembea na sisi wakati ana mke na watoto.

 

WAUNGANA KUMSHITAKI MWALIMU

“Niliumia sana kwa kitendo cha mwalimu kunikatisha masomo, nilienda kuomba msamaha nyumbani na Agnes naye akafanya hivyo. Lakini baadaye tulikaa na kukubaliana kuwa tukamshitaki kwa kuturubuni, kutuzalisha na kututelekeza,” alisema Jovita.

 

WAINGIA KITAA KUMSAKA

Tulienda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha MabiboMpakani kisha kwa kushirikiana na polisi tulianza kumsaka kwenye maeneo aliyokuwa anapenda kukaa na kufanyia kazi.

 

MWALIMU ANASWA

Baada ya kumsaka kwa muda, hatimaye Jumatatu iliyopita tulifanikiwa kumnasa akiwa Mabibo-Makutano na kufikishwa katika kituo hicho cha polisi cha Mpakani ambapo alihojiwa na kisha kuhamishiwa Kituo cha Urafiki.

 

SHANGAZI ASIMULIA

Akizungumza na gazeti hili, shangazi wa Jovita aliyejitambulisha kwa jina moja la Anna, ambaye ndiye aliyekuwa akimsomesha, alisema alisikitishwa sana na kitendo cha mwalimu kumrubuni binti yake na kumzalisha.

 

“Ukweli roho iliniuma sana baada ya kusikia binti niliyemlea na kuamua kumsomesha kwa gharama, anapewa mimba tena na mwalimu wake. Kumbe hakuwa binti yangu peke yake, yupo na mwingine na wote amewapangishia na kuwatelekeza,” alisema shangazi huyo. Kufuatia sakata hilo, Gazeti la Amani, lilimtafuta Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Mulilo Jumanne, ambaye alisema taarifa hiyo bado haijafika mezani kwake na kuahidi kufuatilia.

MWALIMU ATIWA MBARONI
Akishuka ndani ya gari.

 

STORI: RICHARD BUKOS| AMANI

Leave A Reply