The House of Favourite Newspapers

Mwalimu Mkuu Ajiua kwa Kunywa Sumu

MWALIMU Mkuu wa Sekondari ya Mbalamaziwa iliyopo mkoani Iringa, Roida Mbalwa,  amefariki dunia kwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa kwenye mkutano na kiongozi mmoja kutumia vibaya fedha za ujenzi.

 

Mume wa marehemu, Sharif Utenga, amesema kuwa kiongozi huyo aliitisha mkutano wa hadhara kata ya Mbalamaziwa na wananchi kueleza kuchangishwa michango mingi.

 

”Ninachofahamu ni kwamba alikuja kiongozi fulani akazungumza na wananchi wakasema michango imekuwa mingi, ndipo hapo wakaamua kwenda kumkagua Mwalimu Roida, na baada ya ukaguzi ilibainika kuwa kuna hasara takribani milioni 200,”amesema Utenga.

 

Aidha, Utenga amesema kuwa mara kwa mara viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi wamekuwa wakienda shuleni hapo na kukagua ujenzi kwa sababu majengo hayo yanatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge.

 

”Mke wamgu alikuwa akipata presha ya kazi kutoka kwa viongozi waliokuwa wakifika kukagua, walikuwa wakali na kumtuhumu kwa matumizi mabaya ya fedha, alikuwa akiwaambia walimu wenzake kuwa ipo siku atakuja kujiua,” amesema Utenga.

 

Hata hivyo, diwani wa Mbalamaziwa, Zubery Nyamolelo,  amesema mwalimu huyo hajawahi kutuhumiwa kwa lolote.

Comments are closed.