The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mwalimu Mkuu Mbaroni kwa Rushwa ya Ngono kwa Mwanafunzi

0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma wanamshikilia Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Serengeti iliyopo Serengeti mkoani Mara, Baraka Sabi,  kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita katika shule hiyo ili ampatie cheti chake cha kuhitimu.

 

Akiongea na waandishi wa habari jana Jumapili, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo,  alisema wamemkamata mwalimu huyo kwa kushirikiana na mwanafunzi aliyeombwa rushwa ya ngono ambaye ni  mkazi wa Dodoma aliyehitimu mwaka 2016 na alikuwa anataka cheti aombee kazi.

 

“Mwalimu Baraka alimwambia mwanafunzi asipate shida ya kwenda Serengeti yeye ana safari ya kuja Dodoma katika mkutano wa wakuu wa shule na atakuja na cheti.  Walipokutana akaomba rushwa ya ngono ndipo ampe cheti, msichana akaomba udhuru na kuahidi kurejea, kisha akatutonya,” amesema Kibwengo.

 

Ameongeza kwamba baada ya kupokea taarifa hiyo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na mtoa taarifa kabla ya kufanya tendo hilo.

 

Aliongeza kwamba Takukuru walifanikiwa kuchukua cheti hicho na uchunguzi wa awali unaendelea kwa mujibu wa sheria na hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kukamilika.

RUSHWA YA NGONO Ilivyomfikisha Pabaya Mkuu Huyu wa Shule

Leave A Reply