The House of Favourite Newspapers

Mwambusi Hao Azam Halali Yetu

 

Na Khadija Mngwai/CHAMPION/GPL

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia, mtazamo wao wote wanauelekeza katika mechi yao ya Aprili Mosi dhidi ya Azam FC ili waweze kushinda ikiwa ni njia ya kuweza kutetea ubingwa wao.

Yanga inatarajia kuvaana na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu ambapo kila upande unajinadi kuhakikisha unajipanga na kufanya vema kwa kuibuka na matokeo mazuri katika mchezo huo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwambusi amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao zote katika mchezo huo kuhakikisha wanafanikiwa kushinda na kudai kuwa wanatambua kuwa mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa ndiyo maana wanatumia nguvu nyingi katika kujiandaa na mchezo huo kwa kuwa lengo lao ni kutetea ubingwa wao.

“Tunajiandaa ipasavyo kukabiliana na Azam kwani tunahitaji kushinda mchezo huo na tunauchukulia umuhimu wa hali ya juu kuhakikisha tunapata nafasi ya kutetea ubingwa wetu.

Hali ya kikosi ipo vizuri kila mchezaji anaonyesha morali ya hali ya juu kuona anafanikiwa kushinda mchezo huo, sisi kama walimu tunatumia fursa hii kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita ili kuweza kukifanya kikosi kiwe imara na kukaa tayari kwa ajili yamchezo huo,” alisema Mwambusi.

Comments are closed.