Kartra

Mwamuzi Simba vs Yanga Kesho Huyu Hapa

ULE mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenda soka hapa nchini, umewadia ambapo keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Mkapa, Dar, itashuhudiwa Simba wakiikaribisha Yanga.

 

Huo ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili ambapo wakongwe hao wa soka hapa nchini, mechi ya mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya 1-1.

 

Waamuzi watakaochezesha mchezo huo, wamekuwa wakifichwa sana, lakini wawili kati ya wale waliopangwa kuchezesha mchezo wa wa awali, wakitarajiwa kuwepo tena.

 

Awali timu hizo zilitarajiwa kupambana Mei 8, kabla ya kusogezwa mbele kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya ghafla ya muda.

 

Waamuzi wa mchezo wa kwanza walikuwa ni Emanuel Mwandemba kutoka Arusha ambaye alipangwa kuwa mwamuzi wa kati, Hamdan Said (Mtwara) na Frank Komba (Dar) wakiwa waamuzi wa pembeni, huku mwamuzi wa akiba akiwa Ramadhani Kayoko kutoka Dar.

 

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichoongea na Spoti Xtra, kati ya waamuzi hao, Ramadhan Kayoko na na Frank Komba watakuwepo tena, huku Kayoko akitajwa kuwa ndiye atakuwa wa kati.Kayoko anapokuwa kwenye majukumu yake anakuwa mkali na mbabe katika kuendana na matukio huku akiwa mgumu katika kuyumbishwa.

 

Pia Oktoba 25, 2020, KMC 1-2 Yanga, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kayoko alikuwa kati na alitoa penalti ya utata kwa Yanga. Kutokana na maamuzi hayo, Kamati ya Masaa 72 ilimpa onyo kwa kile ilichoeleza kuwa alichezesha chini ya kiwango.

Kwa upande wa Komba, alikuwepo katika mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Novemba 7, 2020.

STORI: MARCO MZUMBE NA WILBERT MOLANDI


Toa comment