The House of Favourite Newspapers

Mwamuzi Simba vs Yanga ni Faida Kwa Simba

0

MWAMUZI wa mtanange wa Yanga dhidi ya Simba kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Shirikisho la Azam (ASFC), Ahmed Arajiga, amechezesha michezo miwili ya Simba ambayo yote wameshinda na kufikia hatua ya  fainali.


Timu hizo zinatarajia
kushuka dimbani keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma ukiwa ni mchezo wa kumtafuta bingwa wa michuano ya ASFC.

 

Takwimu zinaonyesha kuwa mwamuzi, Arajiga ni faida kwa Simba ambapo kwenye michezo miwili ya ASFC aliyochezesha ambayo ni ya Robo fainali na Nusu fainali, Simba wameshinda.

 

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, mchezo uliopigwa Mei 26, mwaka huu.

 

Mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Azam FC, uliopigwa Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Mwamuzi huyo mwenyeji wa mkoani Manyara hajachezesha mchezo wowote wa Yanga kwenye michuano ya Shirikisho la Azam kwa msimu huu.

Leave A Reply