Mwana FA Afika Kileleni Mlima Kilimanjaro

 

WASANII Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’ wameweka rekodi baada ya kuwa wasanii pekee ambao wamefanikiwa kufika kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro kati ya wasanii 30 ambao walianza safari hiyo kwenye Kampeni iliyofahamika kama HK Kili Challenge.

 

Kampeni hiyo iliandaliwa na Waziri wa Maliasili na Maliasili, Dkt Hamis Kigwangalla na ilishirikisha wasanii wa muziki wa kikazi kipya pamoja na wale wa Bongo Muvi.

FA amefanikiwa kufika kileleni akiwa na picha ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli jambo ambalo ni la kipekee kati ya watu waliopanda mlima huo.

 

Akizungumza mara baada ya kurejea, FA alisema: “Najisikia vizuri sana japo haikuwa mashindano lakini tuliamua kuutangaza mlima wetu baada ya baadhi ya watu kusema ni wao.

Ila nashukuru nimeweza kufika Uhuru Peak wengi wamepambana wameshindwa, tujifunze kupenda vyetu na tunamshukuru Waziri Kigwangalla kwa kampeni.” Baadhi ya wasanii ambao walishindwa kufika kileleni ni Diamond Platiumz pamoja na Steve Nyerere.


Loading...

Toa comment