The House of Favourite Newspapers

MWANA: NGUO ZA HESHIMA NDO’ KILA KITU

MWANA-DASHOSTI wa Bongo Movies, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ amefunguka kuwa kitendo cha Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kupiga marufuku mastaa wa kike kujiachia nusu utupu, ndiyo kila kitu katika kurudisha hadhi iliyopotea ya sinema za Kibongo.

 

Mwana alisema kuwa, baadhi ya mastaa, hasa wa filamu wanaojiachia nusu utupu ndiyo waliochangia kushuka kwa sanaa hivyo waziri amefanya jambo la maana kupiga marufuku na kuwachukulia hatua wale ambao wanaendelea kusambaza picha hizo za kihasara kwenye mitandao ya kijamii.

 

“Sijawahi kukaa nusu utupu na sidhani kama itatokea, ninaipongeza sana serikali kwa kupiga marufuku picha za nusu utupu zilizokuwa zikitupiwa mitandaoni na baadhi ya wasanii kwani zinaharibu maadili ya Kitanzania, ninaamini sasa hadhi ya filamu itarudi maana jamii ilitudharau kutokana na mambo kama hayo,” alisema Mwana.

NA GLADNESS MALLYA | RISASI JUMATANO

Comments are closed.