The House of Favourite Newspapers

MwanaFA alivyozindua Mashindano ya Sanaa na Utamaduni ya Mkuu wa Majeshi

0

Dar es Salaam 19 Agosti 2024: Naibu Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA Jana alizindua rasmi mashindano ya Sanaa na Utamaduni ya Mkuu wa Majeshi ambapo vikundi 19 vya Majeshi ya Ulinzi vinashindana katika Sanaa ya muziki wa dansi na ngoma za asili. Baada ya uzinduzi huo Kikundi cha JKT Makotopola na Mwenge Jazz ndiyo walioanza kutifuana.

Akizungumza kabla ya kuzindua mashindano hayo MwanaFA amesema Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuenzi utamaduni wetu ndio maana amekuwa akihudhuria matamasha mbalimbali ya utamaduni ikiwemo lile lililoandaliwa na machifu ikiwemo wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kikundi cha Makotopola JKT kikionesha burudani kwa ngoma ya asili ya mkoa wa Ruvuma.

“Nimefurahi sana kuona jeshi limerudisha sanaa hizi za kitamaduni na ni jukumu letu sote kuulinda na kuuenzi kwa sababu ndio misingi ambayo tumekuwa nayo tangu zamani hivyo tusiruhusu kuingilia na maadui”.

“Basata kama wasimamizi wakubwa wa kazi za sanaa nawapongeza kwa kuwa na wao ni sehemu ya mashindano haya naamini haki itakwenda kutendeka majaji watahakikisha ushindi unapatika kwa kundi linalostahili.

JKT Makotopola Jazz wakiwajibika jukwaani kwenye mashindano hayo.

Nae Meja Jenerali Mbaraka Mkeremy ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhalizi ya Mashindano ya Utamaduni ya Mkuu wa Majeshi, alisema kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Jacob Mkunda aliona ni vyema kurudisha baadhi ya sanaa na tamaduni ambayo yanaonekana kupotea, hivyo aliona ni vyema kurudisha tamaduni ikiwemo ngoma za asili na mbalimbali vya kiasili.

Mwenge Jazz wakifanya yao kwenye mashindano hayo.

Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 19 hadi 30 Agosti 2024, kuanzia saa nane mchana ambapo mgeni rasmi kwenye uzinduzi alikuwa Naibu Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Hamis Mwijuma aliyemuwakilisha Waziri wake, Mhe. Dk. Damas Ndumbaro ambapo yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mh. Dk. Stergomena Lawrence Tax (Mb).

Mashindano hayo yanafanyika Msasani Beach Club ambapo hakuna kiingilio na wananchi wote wanakaribishwa kwenda kujionea mashindano hayo. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN/ GLOBAL PUBLISHERS.

Leave A Reply