The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Ajiua kwa Kukataliwa Urafiki

0

KATI ya kuacha kuwa na marafi ki wa kiume na kufa, unachagua nini? “Nachagua kufa,” ndivyo mwanafunzi wa Kidato cha Pili Shule ya Sekondari ya Kyela mkoani Mbeya, Grace Gowele ‘15’ alivyochagua baada ya kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kupinga agizo la baba yake la kutojihusisha na marafi ki wa kiume.

 

Imeelezwa kuwa, baba wa mwanafunzi huyo aitwaye Majaliwa Gowele, alikuwa mchungu kwa mwanaye kutokana na kile alichohisi kuwa binti yake alikuwa ameanza kujihusisha na masuala ya uasherati pasipo kuzingatia masomo.

 

Akizungumza jana na gazeti hili Sophia Ngoi, mkazi wa Kyela alisema mzazi huyo alikuwa na tabia ya kumcharaza bakora mtoto wake kumuonya aachane na habari za mapenzi, azingatie masomo.

 

“Hata akimkuta mwanaye na mwanafunzi mwenzake wa kiume, alikuwa anamchapa,” alisema Sophia. Aliongeza kuwa, kitendo cha kushushiwa kipigo mara kwa mara, kilimkera mwanafunzi huyo na huenda ndicho kilichosababisha ajinyonge kwa kamba ndani ya nyumba yao. Jirani mwingine wa familia ya marehemu aitwaye Khatibu Msamba, alisema tukio hilo limewashangaza.

 

MWENYEKITI WA KITONGOJI ASIMULIA

Akisimulia kwa masikitiko tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Roma, Michael Mwakibinga alisema ilikuwa saa mbili na nusu usiku, alipopigiwa simu na majirani kuelezwa kuwa, mwanafunzi kajinyonga. “Nilipofi ka eneo la tukio, nilikuta ni kweli.

 

Nikaagiza baba wa mtoto adhibitiwe kwa kuwa alitajwa kusababisha kifo cha mwanaye. “Baadaye niliwapigia polisi simu wakaja kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi na mtuhumiwa wakaondoka naye,” alisema mwenyekiti huyo.

 

Aliongeza kuwa, baada ya baba wa mtoto kutiwa mbaroni na polisi na kufanyiwa mahojiano, aliachiwa kwa dhamana huku akiruhusiwa kuzika mwili wa binti yake.

 

Alisema, wakiwa nyumbani kwa marehemu wakiendelea na taratibu za kuusafi risha mwili wa marehemu kwenda Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa maziko, mama mzazi wa marehemu Grace, Elisia Msilanga pamoja na ndugu zake, wasusia shughuli hizo.

 

“Kitendo cha mama mzazi wa mwanafunzi ambaye alishatengana na mumewe kutoshiriki mazishi, kiliwashangaza wengi na kuzua minong’ono mingi. Mwenyekiti huyo alisema, wao kama viongozi wa mtaa, walimaliza kazi yao hapo, na sasa wameliachia jeshi la polisi ambalo linaendelea na uchunguzi zaidi juu ya kifo cha mwanafunzi huyo.

 

MKUU WA WILAYA ANENA MAZITO

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Claudia Kitta alikiri kuwepo na tukio.

 

“Mtoto huyo inasemekana alikuwa na tabia mbaya za kutembea na wanaume, huku akikutwa na vitu kadhaa vinavyosadikiwa kuwa alikuwa akihongwa na wanaume zake na alipokuwa akionywa, alikuwa mkali.

 

“Hata hivyo, uamuzi aliochukua ni mgumu, nichukue nafasi hii kuwaasa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi. “Kama kuna matatizo ya kifamilia, ni bora kuwashirikisha viongozi wa mtaa au wa dini, ili suluhu ipatikane,” alisema mkuu huyo wa wilaya.

 

HUYU HAPA KAMANDA

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei alipopigiwa simu na mwandishi wetu mara kadhaa ili afafanue kinachoendelea hivi sasa juu ya tukio hilo, hakupokea.

Stori: Ibrahim Yassin, Kyela

Leave A Reply