Mwanafunzi Aliyevamia Ikulu na Kisu, Apigwa Risasi!

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, amepigwa risasi ya bega na polisi baada ya kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.

 

Kibet wenye umri wa miaka 25, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na polisi waliokuwa wakifanya doria katika eneo hilo hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.

 

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena-Mararo, tukio hilo limetokea Jumatatu (juzi) na mtuhumiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta kwa ajili ya matibabu.

 

Siku moja kabla ya tukio hilo kutokea Kibet aliandika katika mtandao wake wa Facebook kuwa atavamia Ikulu ya Kenya, jijini Nairobi.

 

Tukio hilo limezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini humo huku baadhi watu wakiamini huenda mwanafunzi huyo alichukua hatua hiyo baada ya kutumia kilevi kwa sababu mtu aliye na akili timamu hawezi kufanya hivyo.

 

Kwa sasa Kibet anaendelea na matibabu.

 

WATU 10 MATAJIRI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI!


Loading...

Toa comment