The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Darasa la 4 Ajinyonga Baada ya Kulazimishwa Kwenda Shule

MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Osanyui jijini Arusha, Eribariki Lekini (12) mkazi wa mtaa wa FFU adaiwa kujinyonga hadi hadi kufa baada ya baba yake mzazi kumlazimisha kwenda shule.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amethibitisha kutokea tukio hilo, na kudai kuwa mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukining’inia katika nyumba ya Emmanuel Thomas inayoendelea kujengwa.

Kamanda Shana amesema kuwa kulikuwa na ugomvi na baba yake mzazi uliotokana na marehemu kutotaka kwenda shule.

“Kulikuwa na ugomvi kata ya marehemu na baba yake mzazi na ugomvi huu ulikua unatokana na marehemu kutotaka kwenda shule ina maana kwamba marehemu alikua ni mtoro sugu” amesema Kamanda Shanna nakuongeza;

“Tunaendea na uchunguzi wa tukio hili kwa sababu huyu mtoto alitumia eneo ambalo ujenzi unafanyika kufunga kamba juu ya dari,”

Comments are closed.