The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Mtanzania Ashiriki Onesho la Ubunifu Ikulu-Marekani

0

steve3

Stephen Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)

April 13, 2016, Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la mwisho katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za sayansi ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule za awali, msingi hadi za sekondari kutoka States mbalimbali za Marekani.

Kwa miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa akifadhili onyesho hilo lijulikanalo kama White House Science Fair ambalo limekuwa likifanyia katika Ikulu yake (White House) lengo likiwa ni kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, hisabati, teknolojia na ufundi ( STEM)na hivyo kuibua vipaji vya ubunifu m iongoni mwa wanafunzi ( young inventors).

Katika onyesho hilo la Aprili 13 jumla ya wanafunzi 130 walishiriki baada ya kukidhi vigezo vya kuingia katika onyesho hilo. Miongoni mwa wanafunzi waliopata fursa hiyo adhimu ya kushiriki baada ya kukidhi vigezo ya ubunifu wao ni mwanafunzi mtanzania Stephen Wilfred Mwingira ambaye pamoja na wenzake wawili Armo Halwah na Wendy Ni wanaosoma Baruch College Campus High School ya jijini New York, wamebuni kifaa cha gharama nafuu (vacuum cleaner) kinachoweza kutumika katika kusafisha njia za reli za chini ya ardhi ( Subways).

Stephen Mwingira na timu yake, walipata fursa ya kuelezea na kuonyesha mbele ya Rais Obama namna gani kifaa walichobuni ( Vacuum Cleaner) kinavyoweza kufanya usafi kwa kufungwa kwenye treni na hivyo kusaidia katika kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa katika mazingira ya usafi na hivyo kupunguza gharama za usafishaji.

Katika miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi amejipambanua kama mpenzi na shabiki mkubwa wa sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa motisha na kivutio kikubwa kwa walimu, wanafunzi, wafadhili na wataalamu waliobeba katika masuala ya sayansi, teknolojia na hesabu.

Kila mwaka State dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la maonyesho ambapo wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni au kutoa maelezo ya kisayansi ya namna ya kutatua tatizo Fulani kwa kutumia teknolojia nafuu.

Katika kutambua mchango wa Rais Barack Obama katika kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, Ikulu ya White House imetangaza kwamba Kampuni ya Oracle inayojihusisha na masuala ya teknolojia ya Komputa katika miezi kumi na nane ijayo itawekeza dola za kimarekani 200 milioni kwaajili ya masomo ya sayansi ya computa kwa wanafunzi wa kimarekani.

Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada ya kuhitikishwa kwa onyesho lake la mwisho, Rais Barack Obama amesema, mara zote ambazo ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye kiu na ari ya kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na mara zote amejiona kama anayepungukiwa na kitu kutokana kile anachojifunza kutoka kwa wanafunzi hao.

“Nimeweza kujionea ubunifu wa hali ya juu, kiu, na hamu ya watoto na vijana wetu wataalamu wa kesho wa taifa letu la marekani. Ipo siku huko mbeleni nitajivunia pale ambapo miongoni mwa vijana wetu hawa watakapoweza kubuni tiba ya kansa.

Nitaangalia nyuma kwa fahari kubwa kwamba niliwawezesha vijana hawa kuibua vipaji vyao ”. Akasema Rais Obama kwa furaha huku akiwashukuru wale wote ambao kwa miaka sita mfululizo wamewezesha kwa namna moja ama nyingine kufanyika kwa onyesho hilo.

Chanzo: Michuzi

Leave A Reply