The House of Favourite Newspapers

Mwanahabari wa DW Adaiwa Kulishwa Sumu

0

Deokaji Makomba ambaye ni Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa Hospitalini hapo akiwa hajitambui.

Alikutwa akiwa amepoteza fahamu ndani ya basi la Ally’s. Imeelezwa kuwa alikuwa umelala usingizi mzito na ikabainika kuwa ameibiwa mizigo yake.

Mwandishi huyo alitoka Jijini Mwanza kwa basi hilo na ameeleza kuwa alipewa vipande vya Biskuti na abiria aliyepandia njiani na ndipo akapoteza fahamu.

Mwanahabari huyo licha ya kueleza kuwa anaendelea vizuri lakini amekiri kuwa hana nguvu na bado anahitaji kulala zaidi ili kupumzisha mwili wake.

Leave A Reply