The House of Favourite Newspapers

Mwanahabari wa Ufaransa Aliyeshikiliwa na Wanamgambo Mali kwa Miaka Miwili Arejea Nyumbani

0
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amkumbatia mwanahabari Olivier Dubois muda mfupi baada ya kufika kwenye uwanja wa ndege wa Villacoublay karibu na Paris. March 21, 2023.

Mwanahabari Olivier Dubois mwenye umri wa miaka 48 kutoka Ufaranasa Jumanne amerejea nyumbani baada ya kushikiliwa kwa karibu miaka 2 kwenye eneo la Sahel.

Mwanahabari huyo alilakiwa na familia yake pamoja na rais Emmanuel Macron, kwenye uwanja mmoja wa ndege karibu na mji mkuu wa Paris. Dubois akiwa na mfanyakazi wa kutoa msaada Jeffery Woodke mwenye umri wa miaka 61 kutoka Marekani walikamatwa kusini magharini mwa Niger Okotoba 2016, na waliwasili kwenye mji mkuu wa taifa hilo wa Niamey Jumatatu baada ya kuachiliwa huru.

Olivier Dubois akisalimiana na familia yake.

Video iliyotolewa awali na watu waliokuwa wamemshikilia inasema kwamba walikuwa ni kutoka kundi la Support Group for Islam and Muslims, GSIM, ambalo linajumuisha makundi ya kigaidi ya Sahel, na linalohusishwa na lile la Al-Qaeda. Dubois alikuwa akiishi nchini Mali tangu 2015 wakati akiwa mwanahabari huru wa gazeti la Ufaransa la Liberation, pale alipokamatwa. Hakuna taarifa za kina zilizotolewa kuhusu Dubois na mwenzake Woodke.

WAZIRI UMMY ATOA TAMKO UGONJWA ULIOUA WATANO KAGERA – ”HAUNA TIBA, NI MARBURG”…

Leave A Reply