Mwanahamisi wa Simba Queens Kwenda Morocco Leo
Leo Machi 13, 2021 Jumamosi nahodha na straika wa Simba Queens na Twiga Stars, Mwanahamis Omary anatarajia kusafiri kwenda nchini Morocco.
Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema kila kitu kuhusu yeye kuondoka kipo tayari kinachosubiriwa ni siku na muda wa kusepa hapa nchini ufike.
Championi lilimtafuta Mwanahamisi ili kujua mpango huo ulipofikia ambapo alisema: “Ukweli hilo dili lipo, lakini meneja wangu ndiye mwenye uwezo wa kuzungumza ukweli nini kinaendelea.
”Kwa upande wake, Meneja wa Simba Queens, Seleman Erassy Makanya alisema: “Subiri kila kitu kikamilike kisha nitakupa majibu ya nini kipo juu ya dili hilo, kwa sasa achana na mambo ya mitandao.”
Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam