The House of Favourite Newspapers

MWANAHAMISI: YANGA NIMEWAFUNGA KWA MAKOSA YAO

Mshambuliaji wa Simba Queens, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ (kulia).

MSHAMBULIAJI wa Simba Queens, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ ameweka rekodi mpya katika medani ya soka la wanawake kufuatia kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne katika mchezo wa Simba na Yanga nchini. Mwanahamisi alifunga mabao hayo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess.

Mwanahamisi Omary (kushoto) akifanya yake.

Katika mchezo huo uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Karume ambao umekuwa wa kwanza katika soka la wanawake tangu kuanzishwa kwake huku Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 7-0.

 

Ushindi huo umesababisha Simba kufi kisha pointi 13, nyuma ya ligi hiyo JKT Queens kabla ya mchezo wa jana jioni dhidi ya Simba, walikuwa wanaongoza wakiwa na pointi 15 baada ya wote wakiwa wamecheza mechi tano kabla ya Jumatano kukutana kwenye ligi hiyo.

Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili limefanya mahojiano maalum na Mwanahamisi maarufu kama Gaucho akifananishwa na mshambuliaji wa zamani wa Brazil na Klabu ya Barcelona, Ronaldinho Gaucho juu ya mabao hayo.

 

UNAZUNGUMZIAJE KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KUIFUNGA YANGA HAT TRICK?

“Binafsi naona kuwa na Simba na Yanga kwenye soka la wanawake hili limekuwa ni jambo zuri kwa kuwa tunahamasisha kesho kuwepo na Lipuli, Azam ya wanawake itakuwa ni kitu kikubwa. “Lakini kwenye upande wa kilichotokea kwenye mchezo kwangu ni historia tayari ikiwa kucheza Simba pamoja na kuifunga Yanga. “Naamini imekuwa ni furaha kwa kuwa nimefanikiwa kufunga hat trick lakini inakuwa changamoto kubwa kwangu kuendeleza kiwango hiki katika kila mchezo.

 

ULITARAJIA UTAFUNGA HAT TRICK?

“Unajua Yanga ni timu nzuri halafu kila timu inayoingia kwenye ligi kuu ni bora ila tu ni suala la maandalizi kwa sababu mpira wa wanawake una changamoto nyingi mno. “Lakini kuhusu kufunga hat trick sikuwa na wazo hilo ila nilijua kwamba naweza nikafunga pengine bao moja au mawili lakini sasa nimeweza kufunga mabao manne kwangu siyo jambo dogo.

LIGI YA WANAWAKE INA CHANGAMOTO GANI?

“Changamoto ni kubwa ila hakuna anayejua kwa kuwa watu wanatuona tu uwanjani tukicheza ila niwashukuru TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) licha ya changamoto zilizokuwepo lakini bado w a m e k u w a wakiendelea kuandaa ligi hii kwa udhamini wa Serengeti. “Ukiangalia upande wetu bado kuna tatizo kubwa la udhamini kwa kuwa makampuni mengi yamekuwa yakizitolea macho ligi za wanaume tofauti na sisi hali ambayo imepelekea timu zinazoshiriki ligi zikiwa kwenye mazingira magumu.

 

HII NI HAT TRICK YAKO YA NGAPI? “Kiukweli katika msimu huu hii ndiyo hat trick yangu ya kwanza ila natarajia mengi zaidi huko mbele kadiri Mungu atakavyonijalia kwenye ligi hii

 

UNAMZUNGUMZIAJE KINARA WA UFUNGAJiI KUTOKA JKT QUEENS?

”Kwanza msimu huu nimeshafunga mabao saba tayari lakini ukija upande wa Fatuma Mustapha ambaye ndiyo anaongoza kwa kufunga msimu huu kwangu ni mchezaji mzuri sana na siyo yeye peke yake hadi Asha Rashid ‘Mwalala’ namuheshimu pia. “Unajua Fatuma ndiyo alikuwa ‘role model’ wangu, namuheshimu kwa sababu timu yao ni nzuri na wapo sehemu mmoja kwa muda mrefu.

 

“Lakini kwa upande mwingine ukiziondoa Simba na Yanga hizi timu nyingine bado zipo kwenye wakati mgumu kutokana na changamoto kibao ndiyo maana wanapokutana na JKT wanakuwa wameshachoka wanapigwa bao nyingi.

 

YANGA UNAWAPA NAFASI GANI MSIMU HUU?

“Kufungwa kwao bao saba leo (juzi) kusiwafanye washushe morali yao chini kwa sababu wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kupambana na wajipange wao na uongozi wao ili waboreshe pale wanapokosea. “Ukiangalia hata Simba msimu uliopita
haikuwa bora kama msimu huu kwa sababu ilikuwa inafungwa hadi mabao tisa sasa na wao wakijua mapungufu yao watakuwa bora na siyo kukata tamaa.

 

MPIRA ULIOPEWA UNAKWENDA KUTUMIA?

“Hapana, huu mpira utabakia sehemu ya kumbukumbu ya maisha yangu, nitauweka ndani kwangu na kila atakayekuja atauona hata mwenzangu akiona ataridhika kwa kile ninachokifanya.

 

UMEPANGA KUFUNGA MABAO MANGAPI MSIMU HUU? “Siwezi sema nitafunga mabao mangapi kwa kuwa ligi ni ngumu na ukiangalia kuna mechi zaidi ya 24 bado hatujacheza ila hapo kuna majeruhi halafu suala la namba.

KUWAFUNGA YANGA BAO NNE PEKE YAKO WALIKUWA WANAKUOGOPA? “Hapana siyo kwamba wao walikuwa wananiogopa ila nimefanikiwa kuwafunga Yanga ni kwa sababu ya makosa yao madogomadogo ndiyo yamepelekea kuwagharimu,” anasema Gaucho.

USIKOSE KUTAZAMA KIPINDI CHA SPOTI HAUSI KWENYE GLOBAL TV ONLINE LEO SAA 10 JIONI.

MAKALA NA IBRAHIM MUSSA

Comments are closed.