Mwanajeshi Ashtakiwa Kumuambukiza kwa makusudi virusi vya Ukimwi mpenzi wake – Video
Mwanajeshi wa zamani wa Afrika Kusini akutwa na hatia ya kutaka kuua na kubaka baada ya kumuambukiza makusudi virusi vya Ukimwi mpenzi wake.
Awali, mwanadada husika kwa jina la Antoinette ambaye pia yupo katika jeshi la nchi hiyo aliposhtaki kwa kuambukizwa HIV makusudi, taasisi ya jeshi la nchi hiyo ilikataa kutoa historia ya taarifa za kiafya za mlalamikiwa Leon Santos Conga na hivyo kusababisha mahakama kuindoa kesi husika mara mbili tangu ifunguliwe 2018.
Lakini mwanadada hakukata tamaa alikomaa akaenda kwenye taasisi binafsi inayojihusisha na mambo ya kimahakama kulalamika kutotendewa haki ndio taasisi husika ikalilazimisha jeshi liweze kutoa rekodi za kiafya za mwanajeshi huyo ambapo rekodi zimeonesha tangu 2007 alikuwa anajijua ana virusi vya Ukimwi na bado alipoanzisha mahusianonl na Antoinette 2016 alimficha kuhusu hali ya afya yake licha ya kwamba walilijadili mapema suala la kiafya kabla hawajakutana kimwili.