The House of Favourite Newspapers

Mwanamitindo wa kiume afariki akiwa jukwaani

 

Mwanamitindo wa kiume Tales Soares  miaka 26 amefariki alipokuwa akifanya onyesho la mavazi katika tamasha la mitindo la São Paulo nchini Brazil.

 

Mwanamitindo huyo ameripotiwa kuanguka baada ya kutegwa na kamba za viatu alivyokuwa amevivaa katika maonyesho hayo.

 

Watu mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo awali walifikiri kuanguka kwake kulikuwa sehemu ya onyesho lake, lakini walishtukia amebebwa kutoka ukumbini hapo na walinda usalama akiwa amezirai.

 

Baadaye alipelekwa hospitali lakini madktari hawakuweza kuyaokoa maisha yake.

 

Kanda za video zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonyesha Soares akitembea kwa mwendo wa madaha kisha akageuka na kuangalia nyuma kabla kisha kuanguka.

Comments are closed.