The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Aliyeng’atwa Na Nyoka Akiwa Haja Kubwa Chooni Asimulia

 

MWANAMKE mmoja nchini Australia “ameruka kutoka kwa kiti cha choo” baada ya kung’atwa na nyoka aina ya chatu.

 

”Nilihisi kama nimedungwa kisu kwenye makalio,  ilikuwa uchungu sana; ghafla nilijikuta nimeruka juu na kukimbilia nje nikiwa nusu uchi, ” Hellen Richards aliviambia vyombo vya habari.

 

Bi Richards, 59, aling’atwa nyoka huyo katika nyumba ya jamaa zake mjini Brisbane mapema wiki hii.

 

Mtaalamu wa kushughulikia nyoka, Jasmine Zeleny, aliyemtoa nyoka huyo kutoka chooni, amesema ni kawaida kwa nyoka kutafuta maji chooni hasa wakati wa msimu wa joto kali.

 

Zeleny amesema Bi Richards ametibiwa na kupewa dawa ya maumivu, akielezea kuwa aina hiyo ya chatu haina simu.

 

 

“Njia ya nyoka huyo kutoka chooni ilizibwa wakati Helen alipokuwa akijisaidia, ndipo akamng’ata akihofia kudhuriwa,” Bi Zeleny aliiambia BBC.

 

Chatu aina ya ‘Carpet python’ hupatikana sana katika pwani ya mashariki mwa Australia.  Huwa hana sumu lakini anapomng’ata mtu inapendekezwa adungwe sindano ya pepo-punda.

 

Wiki za hivi karibuni Australia imekuwa ikishuhudia joto kali ambalo limevunja rekodi ambapo wanyama wengi wa porini wameripotiwa kufa, wakiwemo popo na samaki.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.