The House of Favourite Newspapers

MWANAMKE BIKRA ‘ALIYEFUNGA NDOA’ NA YESU KRISTO AZUA GUMZO

MWANAMKE mmoja, Jesca Hayes (41) amejinunulia mwenyewe shela, ushungi na pete ya ndoa, na kwenda madhabahuni kufunga ndoa, lakini aliposimama altareni kufungishwa ndoa na Askofu, hakuwepo bwana harusi pembeni yake.

 

Alikuwa akifunga ndoa na Yesu Kristo.

Bi Hayes, ni mwanamke bikra aliyejihifadhi ili awe mke wa Mungu, hii ni ada ambayo si ya lazima wanayoweza kufanya wanawake wanaoamini katika ukatoliki kwa kujitoa wakfu miili yao kwa Bwana kwa maisha yao yote.

 

Lakini hata ndani ya Ukatoliki, ada hii inayofahamika kwa Kingereza kama consecrated virgins si maarufu na waumini wachache wanafahamu juu ya mabikra hao. Moja ya sababu ni kuwa ada hiyo iliruhusiwa kwa uwazi na Kanisa miaka 50 iliyopita.

 

Katika sherehe ya wakfu ama harusi, mwanamke bikra ambaye huvaa shela jeupe, hula kiapo cha maisha cha kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na kutokufanya ngono. Wanawake hao pia huvaa pete za ndoa ambayo huwa ni alama ya kufunga uchumba ama ndoa na Kristo.

 

“Mara nyingi naulizwa: ‘Kwa hiyo, umeolewa? Kawaida huwajibu kuwa mimi ni sawa tu na wanawake watawa (masista) wa kanisa, na nimejitoa kwa Kristo kwa moyo wote, tofauti mie naishi nje na watu wa kawaida,” anasema Bi Hayes. “

Mwanamke huyo ni mmoja kati ya “wake wa Kristo” 254 wanaoishi nchini Marekani kwa mujibu wa taasisi yao iitwayo United States Association of Consecrated Virgins (USACV). Wanawake hao wanafanya kazi mbali mbali ikiwemo zima moto, uhasibu, ualimu na wengine ni wafanyabiashara.

 

Duniani kote kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2015 kuna wanawake kama hao 4,000 huku Vatican (makao makuu ya kanisa katoliki) ikisema ada hiyo imekuwa ikipata wafuasi wengi katika miaka ya karibuni kutoka maeneo tofauti ya dunia.

 

Tofauti na masista, mabikra watakatifu ama wake wa Yesu, hawaishi kwenye makao maalumu ya kanisa ama kuvaa nguo maaalumu; wanaishi maisha ya kawaida, wanafanya kazi na wanijetegemea kwenye kuendesha maisha yao ya kila siku.

 

Hakuna ada kama hiyo kwa wanaume ndani ya Kanisa Katoliki.

Ufaransa na Italia wanaongoza kwa kuwa na mabikra watakatifu 1200 kwa ujumla. Nchi nyengine kama Mexico, Romania, Poland, Uhispania, Ujerumani, Argentina na Marekani pia zina wanawake kama hao wengi. Kufikikia mwaka 2020 idadi ya wake wa Kristo inatarajiwa kufikia 5,000.

 

“Mimi ni mwalimu kwa miaka 18 sasa na ninafundisha shule ya sekondari ambayo pia nilisoma,” anasema Bi Hayes, ambaye ni mkaazi wa Fort Wayne, jimboni Indiana, Marekani. [Kabla ya wakfu] Niligundua kuwa sikuwa na wito wa kuhudumia na kuishi katika jamii kama wafanyavyo masista, iwe katika mkusanyiko wa kanisa ama mashirika ya kiutume,” aemsema.

Anapokuwa hayupo shuleni bi Hayes anatumia muda wake mwingi kufanya ibada na toba. Pia huripoti kwa Askofu na mshauri wake wa masuala ya kiroho. “Naishi na jamii ya watu, nipo chini ya parokia ambayo ipo maili mbili kutoka ninapoishi. Nipo tayari muda wote kuwasaidia rafiki zangu na ndugu. Na pia nafundisha lakini juu ya yote hayo napata wakati mtakatifu kwa ajili ya Bwana.”

 

Anasema alishawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi (bila kufanya ngono) lakini mahusiano hayo hayakumtosheleza. “Nilihisi wito wa kuolewa, na hilo ni jambo la asili kwa wanaadamu. Hivyo, nikaingia kwenye mahusiano… lakini sikuwa na yakini.”

TBC 1: Wimbo wa Roma Na Mwasiti Wazua Gumzo Studio za TBC 1!

Comments are closed.