The House of Favourite Newspapers

Mwanamke kusikia maumivu wakati na baada ya tendo la ndoa

0

Happy-couple-bed-008.jpgWAPO ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata furaha, wao wanasikia maumivu, wanaume ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili.

Mwanamke anaweza kukosa kuhisi furaha na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni, ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo la ndoa ambapo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo.

KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO

Maumivu haya hutokea pale mwanamke anapoanza kukutana kimwili na mwanaume na mara nyingi hutokana na uke kuwa mkavu.

Hii inaweza kusababishwa na maandalizi hafifu ya kabla ya tendo lenyewe na matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko wa hamu ya tendo hilo. Kubana kwa misuli ya uke pia nako kunachangia sana ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo kutokana na kumbukumbu mbaya za nyuma.

Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa michubuko na vidonda au maambukizi ukeni mfano kama fangasi za muda  mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono nayo husababisha.

Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri pia huchangia.

MAUMIVU BAADA YA TENDO

Maumivu haya hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa kumalizika. Mwanamke atahisi maumivu makali kwa ndani zaidi ya uke au chini ya tumbo lake. Maumivu haya huwa makali na huchukua muda mrefu kupoa.

Maumivu ya chini na ndani zaidi ya uke huleta hisia kama muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa unazidi kupata maumivu.

Itaendelea wiki ijayo kwenye gazeti hili hili.

Leave A Reply