Mwanamke Mwafrika wa Kwanza Kuajiriwa Shirika la Anga za Juu (NASA)

 

FADJI MAINA amekuwa mwanasayansi wa kwanza kutoka nchini Niger kufanya kazi na Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA).

 

Bi Maina mwenye umri wa miaka 29 alipata shahada ya uzamifu (PhD) mwaka 2016 na alijiunga na shirika hilo maarufu la anga za juu nchini Marekani mwisho wa mwezi uliopita.

 

Ameiambia BBC atatumia kazi yake mpya kurudisha shukurani sio tu nchi yake bali pia kwa bara zima la Afrika.

 

“Nawaasa wanawake wenzangu wasikate tamaa kufikia ndoto zao kwa sababu hakuna mtu angefikiria mwanamke kutoka Niger, au msichana mdogo kutoka Niger, angeweza kufika mahali kama hapa. Siri ni kujiamini na kutafuta mazingira ambayo yatakusaidia kufikia ndoto yako,” alisema katika mahojiano yake na BBC.

 

Toa comment