The House of Favourite Newspapers

Mwanamuziki Nguli Mose Fan Fan Afariki Dunia

MWANAMUZIKI maarufu wa DR Congo Mose Fan Fan (75) amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo nyumbani kwake karibu na barabara kuu ya Thika jijini Nairobi nchini Kenya.

Mtunzi huyo wa wimbo ‘Papa Lolo’ alikuwa gumzo jijini Nairobi wakati wa kurekodi nyimbo mpya na wanamuziki wa Nairobi akiwemo Paddy Makani na Disco Longwa.

 

”Mose alikuwa akicheza Gita na bendi ya Franco Ok Jazz mwaka 1972. Ninamtambua kuwa mchezaji Gita na mwandishi mzuri wa nyimbo barani Afrika. Amekuwa akizuru nairobi mara kwa mara tangu 2015 akishirikiana na na bendi ya Ketebul Music na tabu Osusa”, alisema mshindi wa tuzo ya kuchora wanasesere Paul Kelemba a.k.a Mado kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya.

 

Mashabiki wa mwanamuziki huyo waliomboleza kifo chake muda tu habari zake zilipoanza kusambaa katika vyombo vya habari. Mose alipenda sana kuzuru Nairobi nchini Kenya kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita akitokea  London alikokuwa anakoishi.

 

”Tumeshangazwa na kifo chake na tunafanya mipango ya kumpeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti huku tukiwasiliana na familia yake,” alisema Osusa.

Comments are closed.