The House of Favourite Newspapers

Mwanamuziki Phina Asaini Rasmi Ziiki Media

0
Pichani kutoka kushoto ni D-Fighter (Meneja wa Phina), Ria Nagar (Meneja Kanda, Ziiki Southern Africa), Phina, Arun Nagar (CEO, Ziiki Media) na Jerry Mayenga (Meneja Biashara wa Phina).

 

Mwimbaji na miongoni mwa vipaji vikubwa vinavyokua kwa kasi na kufanya vizuri kutoka Tanzania ‘Phina’ amejiunga rasmi na kampuni kubwa ya usambazaji muziki barani Africa, Ziiki Media.

Makubaliano hayo ya miaka 4 ambayo yamesainiwa leo Januari 25, 2023 nchini Afrika Kusini, yanalenga zaidi kuendeleza kipaji cha mwimbaji huyo, kukuza soko lake la muziki duniani kupitia usambazaji, pamoja na kukuza fursa mbalimbali za biashara ya Muziki.

 

Kwenye uzinduzi rasmi uliofanyika jijini Johannesburg nchini South Afrika, Phina alisema:

“Najisikia mwenye furaha na bahati kuwa miongoni mwa wasanii [wa kike] kutoka Tanzania kupata nafasi ya kipekee kufanya kazi na familia nzima ya Ziiki Media.

 

Ushirikiano uliozaliwa hapa leo ni hatua kubwa sana kwangu kwani hizi ni aina za fursa ambazo nimekuwa nikizitamani kuzifanikisha kwa muda mrefu kwenye kazi [career] yangu. Niko tayari kuiwakilisha Africa kwenye jukwaa mbalimbali huku tukiendelea kuipeleka sanaa na muziki wa Tanzania [Afrika] mbele”.

Kumkaribisha Phina Ziiki Media, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Arun Nagar alisema:
“Kukutana na kipaji kama cha Phina ni nadra sana, uwezo wake wa sauti na kutawala jukwaa ni vitu vya kushangaza na kutamani kuona kwa wasanii wengi zaidi, binafsi nina shauku ya kuona atafanya nini kwenye jukwa zingine.

 

“Sina shaka na uwezo wake wa kimuziki na nina imani ushirikiano wetu utadhibitisha mengi zaidi ambayo bado hatujayashuhudia kutoka kwake. Nina imani kubwa sana na safari hii na tunafurahi sana kumkaribisha kwenye familia ya Ziiki”.

 

Phina, mwenye ndoto ya kuwa mwimbaji na miongoni mwa watumbuizaji wakubwa duniani tayari amekuwa akijitengenezea heshima hiyo kwenye jukwaa kubwa za burudani nchini Tanzania ikiwemo Fiesta na Mziki Mnene.

Phina anatarajia kuachia kazi mpya tatu Febuari hii, zitakazoshirikisha Mwanamuziki mkubwa barani Afrika.

 

Leave A Reply