MWANAMUZIKI WA INJILI AJIBU ISHU YA KUTEMBEA NA RAMMY GALIS

Image result for irene robert tembea

BAADA ya kufanya vizuri katika soko la ndani na nje ya nchi, mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini, Irene Robert, ameachia wimbo mpya unaoitwa Tembea, ambao kwa sasa unafanya vizuri.

Kwenye video ya wimbo huo ambao umebeba ujumbe wa kuwatia moyo wale wote waliokata tamaa kutokana na matatizo mbalimbali, ameshirikishwa muigizaji Rammy Galis, kama Video King, jambo ambalo limezua gumzo mitandaoni watu wakihoji kulikoni video ya Injili ashirikishwe muigizaji wa Bongo Muvi au wawili hao ni wapenzi?

Image result for irene robert tembea
Akizungumza na Global Publishers, Irene, amesema si dhambi kwa watumishi wa Mungu au waimbaji wa Injili kushirikiana na watu wengine ambao si waumini wa dini ya Kikristo au waigizaji, hivyo hajaona tatizo lolote kumshirikisha Rammy kwenye kazi yake kwani ni kijana mwenye muonekano mzuri wa kufaa kuonekana kwenye video yake, na wala hawana uhusiano wowote wa kimapenzi..

Kabla ya kuacha wimbo wa Tembea, Irene, aliwahi kutamba na nyimbo zake nyingine, kama vile Unashuka, Nianze na Wewe na Kishindo .

Loading...

Toa comment