The House of Favourite Newspapers

Mwanariadha Simbu Atua Dar na Dhahabu Yake Mkononi

simbu-1 Ibrahim Mussa na Denis Mtima

KATIKA hali ya kushangaza, mwanariadha Alphonce Felix Simbu, leo amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar na kujikuta katika wakati mgumu kufuatia mtu aliyetakiwa kumpokea kuchelewa kufika na badala yake akapokelewa na madereva wa taksi wanaofanya shughuli zao uwanjani hapo.

simbu-3Mwanariadha Alphonce Felix Simbu alipowasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar.

Simbu ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya mbio za Mumbai Marathon zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini India, amekuja jijini Dar akitokea Arusha.

simbu-2Global Publishers ambalo lilikuwepo uwanjani hapo wakati Simbu amewasili majira ya saa 11 jioni, lilimshuhudia akihangaika huku na kule kumtafuta mwenyeji wake ambaye alikuja kutokea baada ya kupita takribani dakika 15.

simbu-4

Akihojiwa na wanahabari.

Wakati anamtafuta mwenyeji wake, ndipo wakatokea madereva taksi, wakamchukua na kumuweka pembeni kwa takribani dakika kumi huku akisikika akisema anashangaa ni kwa nini mwenyeji wake hakufika kwa wakati.

Wakati akiwa na madereva hao aliendelea kuwasiliana na mwenyeji wake ambaye alifika baada ya kupita zaidi ya dakika 15, wakapanda gari na kuondoka eneo hilo.

simbu-5Simbu akiwa na dereva wa Kampuni ya Global Publishers, Evans Masambaji wakati wa kumpokea.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday, kesho Ijumaa mwanariadha huyo anatarajiwa kufanyiwa tafrija ya kupongezwa kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar na wadhamini wake, Kampuni ya Multichoice Tanzania.

Comments are closed.