The House of Favourite Newspapers

Mwanariadha Wa Kenya Kelvin Kiptum Afariki Katika Ajali Ya Gari

0
Kelvin Kiptum

MWANARIADHA wa mbio za Marathon kutoka Kenya, Kelvin Kiptum na kocha wake raia wa Rwanda Garvais Hakizimana wamefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Kaptagat kando ya barabara ya Elgeyo Marakwet-Ravine Nchini Kenya.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili saa 11 jioni imemhusisha Kiptum ambaye alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Premio ikiwa na abiria wawili, Garvais na mwanamke aliyejulikana kama Sharon Kosgey wakielekea Eldoret.

Sharon amenusurika akiwa na majeraha mabaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Racecourse kwa matibabu huku miili ya mwanariadha huyo na kocha wake ikipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Racecourse.

Mwanariadha huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 24 alipoteza udhibiti wa gari hilo na kupelekea kuacha njia na kugonga mti mkubwa kabla ya kutua kwenye mtaro umbali wa mita 60.

Leave A Reply