The House of Favourite Newspapers

Mwanauchumi wa Australia aliyefungwa Jela kwa Kosa la Kuvujisha Siri za Nchi Akana Kosa

0
Sean Turnell

MWANAUCHUMI anayejulikana kwa jina la Sean Turnell, kutoka nchini Australia alikuwa serikalini kipindi cha uongozi wa Rais wa Myanmar Aung San Suu Kyi, aliyepinduliwa na Jeshi mwaka jana.

 

Mwanauchumi huyo, ambaye alikuwa ni mshauri wa kielimu na kiuchumii   kipindi cha uongozi wa Aung San Suu Kyi ambaye alizuiliwa mwaka jana baada ya Jeshi kuchukua mamlaka ameweza kusema katika mahakama ya kijeshi kuwa hausiki na tuhuma zinazomkabili.

 

Sean Turnell, kutoka katika Chuo kikuu cha Macquarie huko Sydney alishtakiwa na Aung San Suu Kyi kwa makosa ya kuvunja sheria rasmi ya siri ya nchi.

 

Turnell alikamatwa siku tano baada ya Mapinduzi mnamo February 1 mwaka jana, ambapo kwa sasa anazuiliwa gerezani huko Naypyidaw pamoja na watu watatu kati ya wajumbe wake wa zamani.

Aliyekuwa Rais wa Myanmar Aung San Suu Kyi

Afisa wa kisheria nchini humo anayefahamu kesi hiyo siku ya Alhamisi aliliambia Shirika la Habari la Associated Press kwamba Turnell alikanusha tuhuma zinazomkabili.

 

Melezo kamili hayakupatikana kwa sababu mawakili wake wamezuiliwa kuzungumzia kesi hiyo.

 

Afisa huyo ambaye alitaka kutotajwa jina amesema kuwa Turnell na wenzake walionekana kuwa na Afya njema huko gerezani.

Mwanauchumi Sean Turnell

Pia maelezo kamili ya makosa yanayoshtakiwa hayajawekwa wazi ingawa Televisheni ya Taifa ya Myanmar wakati ikitoa taarifa za kiserikali ilisema kwamba mwaka jana Turnell alikuwa na uwezo wa kupata taarifa za siri za hali ya kifedha na alijaribu kukimbia nchi.

 

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao

 

Leave A Reply