Mwanaume Aaga Dunia Baada ya Kufanya Mapenzi kwa Mizunguko Saba

MWANAUME mmoja aliyefahamika kwa jina moja tu la Davy amefariki wakati akiwa kwenye mashindano ya kufanya mapenzi na mwanamke aitwaye Loveth nchini Nigeria .

 

Baada ya mabishano ya muda mrefu baina ya wawili hao Davy aliamua kumpeleka Loveth kwenye hoteli moja iliyopo Ikotun, Lagos kwa ajili ya kuthibitisha nani ana uwezo wa kufanya mapenzi zaidi.

 

Mwanaume huyo pia aliahidi kumpa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 300,000 Mwanamke huyo kama angemshinda katika tendo hilo.

 

Inaelezwa kuwa Davy aliimudu vyema mizunguko ya awali kabla ya kuzidiwa na kufariki akiwa kwenye mzunguko wa saba.

 

Loveth aliomba msaada kwa Meneja wa hoteli hiyo ambaye alimpeleka katika Kituo cha Polisi cha Ikotun huku mwili wa Davy ukipelekwa Hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Dah! TEMBO ni HATARI Jamani, AMEUA Mtu SHAMBANI, RPC Aonya!


Toa comment