The House of Favourite Newspapers

Mwanaume Anusurika Kukatwa Mkono Baada ya Kung’atwa na Pundamilia Anayemfuga

0

 

Mwanaume mmoja nusura apoteze mkono wake baada mmoja kati ya pundamilia anaowamiliki, kumgeuzia kibao na kumng’ata mkono, tukio lililotokea Circleville, Ohio nchini Marekani.

Katika video inayosambaa kwa kasi mitandaoni, mwanaume huyo anasikika akipiga simu ya dharura akiwataarifu polisi kwamba ameng’atwa na pundamilia wake.

Muda mfupi baadaye, maafisa wa polisi wakiwa kwenye magari kadhaa, waliwasili kwenye shamba la mwanaume huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 72 na kushuhudia jinsi pundamilia huyo alivyokuwa akiendelea kuleta fujo.

 

 

 


Licha ya polisi kufyatua risasi hewani na kupiga ving’ora ili kumfukuzia mbali pundamilia huyo, bado aliendelea kuleta matata, hali iliyowalazimu kumpiga risasi ya kichwa na kumuua.

Mwanaume huyo akasaidiwa na maafisa hao kuelekea kwenye gari la kubebea wagonjwa ambako alikimbizwa hospitali ambako anaendelea kupatiwa matibabu.

Polisi wa Pickaway County, wanasema walipofika eneo la tukio walimkuta mwanaume huyo akiwa amelala chini, damu nyingi zikimtoka.

Luteni wa Polisi, Johnathan Strawser ameeleza kwamba mwanaume huyo amekuwa akifuga pundamilia takribani saba kisheria, ambao wamehifadhiwa kwenye eneo lililozungushiwa uzio.

Nchini Marekani, wananchi wa kawaida wanaruhusiwa kufuga wanyamapori wasio na madhara kwa binadamu baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.

Leave A Reply