The House of Favourite Newspapers

Mwanaume kuwahi kufika kileleni

0

Happy-couple-bed-008.jpgKATIKA kitendo ambacho wanaume wengi hawakipendi vijulikane na wenzi wao ni tatizo la kuwahi kufika kileleni. Kila mwanaume hupenda aonekane ni rijali au mwanaume kamili mwenye uwezo wa kushiriki tendo la ndoa bila shida yoyote.

Imezoeleka katika jamii yetu kwamba, ikiwa mwanaume atakuwa ana tatizo la kuwahi kufika kileleni, anaweza akatangazwa mtaa mzima kila mtu ajue. Hali hii husababisha aibu kubwa na fedheha.

MWANAUME HUJIHESABIA HAFAI

Katika mazingira kama hayo, mwanaume mwenye tatizo hilo hata kama mwenzi wake amemtunzia siri, atahisi kuwa hafai.  Hali hii humfanya kila anapopata hamu ya kushiriki tendo la ndoa aogope kushiriki na mwenza wake kwani ataaibika.

Tumeangalia jinsi tatizo hili linavyoisumbua jamii yetu na pia tumejua kuwa, mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa si jambo la kawaida ni tatizo linaloweza kutibika.

SI LAZIMA DAWA ZA HOSPITALI

Wengi wanatarajia kuambiwa wameze dawa fulani ili kuondokana na tatizo hilo. Kama una tatizo hilo ni vema ukawaona matabibu kwa ushauri na uchunguzi ili kujua chanzo cha tatizo na upate matibabu.

Ni vyema kwa wanaume wenye tatizo hilo washirikiane na wake zao ili kuliondoa. Katika nchi zilizoendelea, wataalamu wamekuwa wakigundua dawa na vifaa tiba vipya vya kuondoa tatizo hili na vingi bado ni vya bei kubwa au vinapatikana kwa shida. Vipo ambavyo vimeonesha mafanikio makubwa. Mifano ya vitu hivyo ni Suction Vibrators, Desire Creams na Erection Drugs.

HII NDIYO HABARI NJEMA

Habari njema ni kwamba tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa mimea tiba na matunda tiba ya kawaida ambayo ipo katika mazingira yetu yanayotuzunguka.

Utafiti umeonesha kuwa tunachokula ndicho kinachotujenga na kutufanya tuwe watu wa aina gani (you are what you eat).

Vyakula tunavyokula vina mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa afya zetu hivyo ni muhimu kuwa makini katika kuamua tule nini na tunywe nini.

Leave A Reply