The House of Favourite Newspapers

Mwanza: Aliyekufa kwa ‘Kujirusha Ghorofani’, RPC Aanika Ukweli – Video


Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limekanusha taarifa ya mtu aliyedaiwa kufariki dunia kwa kujirusha kutoka kwenye ghorofa ya mwisho katika Jengo la Hoteli ya Gold Crest.

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, ACP Jumanne Murilo amesema katika uchunguzi wa awali umebaini hakuna jeraha lolote wala damu kwenye mwili wa marehumu huyo, jambo ambalo si la kawaida kwa mtu aliyejirusha kwenye ghorofa, tena refu kiasi kile.


Muliro ametoa wito kwa wananchi kutoendelea kusambaza habari ambazo hazina ukweli wowote, hivyo polisi inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mtu huyo, na taarifa zikikamilika watazitoa kwa umma.

 

Mtu huyo amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa kujirusha kutoka katika ghorofa ya mwisho ya jengo hilo, liliyopo jijini Mwanza karibu na Uwanja wa Nyamagana, leo, asubuhi, Mei 13 2019.

MSIKIE KAMANDA MURILO AKIZUNGUMZA

Comments are closed.