The House of Favourite Newspapers

Mwanza Kuwa Kitovu cha Biashara

0

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema sababu za Serikali kuimarisha huduma za kiuchumi mkoani Mwanza kwamba inalenga kufanya mkoa huo kuwa kituo kikuu cha biashara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

 

Akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mkuyuni jijini Mwanza leo Jumatatu Juni 14, 2021  akiwa njiani kwenda wilayani Misungwi, Rais Samia amesema hata ujenzi wa ofisi ya kisasa ya Benki Kuu (BoT) jijini Mwanza kwa gharama ya zaidi ya Sh42 bilioni imejikita katika lengo hilo.

 

Katika kutekeleza mikakati hiyo, Serikali inaimarisha huduma za kifedha na kijamii ambapo tayari zaidi ya Sh39.7 bilioni zimetengwa kwa ajili ya  ujenzi wa stendi kuu ya mabasi eneo la Nyegezi na soko kuu.

 

“Ni nia ya Serikali kuona Mwanza inakuwa kituo kikuu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki,” amesema Rais Samia.

 

Akizungumza baada ya kupewa fursa ya Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia Mei, 2021 Mkoa wa Mwanza umeokoa zaidi ya Sh3.9 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu.

 

“Kati ya fedha hizo Sh500 mlioni ni kwa ajili ya utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi na sekondari Mkoa wa Mwanza,” amesema Mwalimu

Leave A Reply