visa

PIKIPIKI YASABABISHA BASI LA ABOOD KUPINDUKA

Muonekano wa Basi la kampuni ya Abood baada ya kupata ajali leo.

BASI  la kampuni ya Abood linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Mwanza limepata ajali mapema leo  Agosti 9, 2019, asubuhi maeneo ya Mkolani jijini Mwanza.

Inadaiwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha pikipiki kuingia barabarani bila ya tahadhari, hivyo kusababisha dereva wa basi kupoteza mwelekeo.

Taarifa za awali zinasema kuna kifo cha mtu mmoja ambaye ni dereva wa pikipiki huku watu kadhaa wakipata majeraha.

Mwonekano wa pikipiki inayodaiwa kusababisha ajali.
Toa comment