The House of Favourite Newspapers

Mwenezi Makalla na Mlezi wa Dar AanzIA Ukaguzi wa Mradi wa Maji Bangulo wa Bil 39

0
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu. Amos Makalla ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Dar es salaam (kichama) ameanza ziara ya kufanya kukagua na kufanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi katika Majimbo 6 ya Ukonga, Segerea, Kibamba, Ubungo, Kawe na Kinondoni.
CPA Makalla amekagua Mradi wa Maji eneo la bangulo Jimbo la Ukonga Wilaya ya Ilala Mradi Wenye ujazo wa Lita Milioni 9 na kugharimu Bilioni 39 ambao utachukua Maji kutoka Ruvu juu na kuhudumia Dar es salam kuanzia Kinyerezi, Kipunguni, Mwanagati na Ilala kwa Ujumla mpaka Temeke yaani tutamaliza kabisa kero ya Maji.
Mwenezi amesema tumpongeze Mwenyekiti wetu na rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumtua Mama kichwani ndoo kwani Mradi huu unakwenda kumaliza shida ya Maji Dar es salam na Sisi Wasaidizi wake tunapita kuona kazi kubwa anavyofanya .
🗓️07 Julai, 2024.
#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee
Leave A Reply