The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti Jumuiya Ya Wazazi CCM Dar Afanya Ziara Wilayani Ubungo, Atoa Maagizo Kwa Viongozi

0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said amesema kipindi cha Wazazi Super Cup ni kipindi cha kuingiza wanachama wapya na anategemea kupata tathmini ya wanachama wapya wa Jumuiya ya Wazazi baada ya Wazazi Super Cup.

Ameyasema hayo leo Mei 13,2023 wakati akifanya ziara katika Wilaya ya Ubungo na Kamati Tekelezi ambapo wamekutana na viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo.

Sehemu ya wanachama wa CCM wakimsikiliza kiumakini Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar, Bi Khadija Said.

Aidha Bi.Khadija amesema Kata ambazo wanaenda kucheza Wazazi Super Cup ametaka wenyeviti wa mtaa na madiwani washirikishwe kwani viongozi hao licha ya kuwa wanadhamana ya kiserikali wengine wamekuwa na uwezo hivyo ni rahisi kwenda kudumisha mahusiano kushirikiana na viongozi wetu.

Pamoja na hayo amesema kuwa Katika kipindi hiki ambacho tunakwenda kufanya Wazazi Super Cup wamezindua kampeni ya Ukatili wa Kijinsia ambapo wanaenda kuongelea na kupiga vita ukatili wa kijinsia lakini pia wanaenda kuongelea malezi chanya kwa wazazi na watoto wetu kwani wazazi ndo chanzo cha mambo mengi yanayoendelea sasa katika jamii yetu;

Shamrashamra za vijana kwenye ziara hiyo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa ligi ya mpira wa miguu iliyoitwa Wazazi Super Cup.

“Sisi wazazi ndo tunakumbatia marafiki sio, sisi ndo tumeitambulisha kigodoro na kukaribisha mengine turudishe mila na tamaduni na utambulisho wa Mtanzania tukiannza na sisi wazazi wenyewe kwanza tujue nini maana ya kuwa mzazi na nini maana yakuwa mlezi”. Amesema Bi.Khadija

Kwa upande wake Katibu Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo Bw.Gaus Kampendeza amesema Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ubungo imeweza kutatua migogoro inayojitokeza ndani ya chama kwa baadhi ya viongozi na kuleta suluhu pia wamekuwa wakitembea kwenye ofisi za kata kuhakikisha wanahamasisha maadili mema ili kulinda jamii yetu kupitia mila na tamaduni za Mtanzania.

Leave A Reply