The House of Favourite Newspapers

MWENYEKITI UVCCM AWACHANA CHADEMA – VIDEO

Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM TAIFA, Kheri James amekisifia chama chake cha CCM na kusema watashinda chaguzi katika majimbo ya Kinondoni na Siha kwani wanaamini watu waliowateua wanauwezo mkubwa na wanakubarika huku wakichagizwa na uwajibikaji mzuri wa chama hicho.

“Chadema wametuletea mtu wa kushindwa, alishindwa Zanzibar, akashindwa Ubunge wa Afrika Mashariki, sasa hivi wamemleta kwetu, tutamshinda tena. Chadema wamekua wakimweka Salum Mwalimu kama chambo ili aangushwe wenyewe waendelee kuwepo, tutashinda kwa kwa kishindo,” alisema Kheri.

Ameyasema hayo kwenye kongamano la vijana lililo andaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, lililo fanyika katika ukumbi wa Urafiki Social Hall, huku akiwataka vijana kuwajibika nakuji tuma kufanya kazi.

Aidha, amewataka vijana kwa kufanya kazi nakuacha kutumika katika mambo ya uchochezi. Hata hivyo amewasisitiza vijana kukumbuka nyumba huku akisema wengi wao husahau walipo toka nakuwataka kujituma nakufanya kazi kwa bidii.

Comments are closed.