The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti wa CCM, Dar Afungua Semina ya Siku Tatu ya Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Dar

0
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar, Abbas Mtemvu akifungua mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya Utekelezaji yaliyoanza jana katika Hoteli ya Stars Breeze Kigamboni jijini Dar.

Viongozi wa Kamati ya Utekelezaji wametakiwa kuendeleza mshikamano na ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinatendeka kupitia Ilani ya CCM ili wanachama na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na imani na chama hicho.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini kusikiliza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.

Ameyasema hayo jana, Januari 12,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu wakati akifungua Semina ya Siku tatu ya Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar, Abbas Mtemvu akisisistiza jambo alipokuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo (hawapo pichani).

Amesema kuna umuhimu wa viongozi wa chama hicho kuhakikisha kamati ya Siasa kutoa hamasa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha chama hicho kinafanya vizuri katika chaguzi zijazo.

Aidha amewataka viongozi hao kushuka kwenye kata, wilaya na matawi kutoa elimu kuhusu masuala ya chama hasa Ilani ya Chama na utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa wa Dar es Salaam.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Adam Ngallawa akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.

Amesema kuna changamoto ya upatikanaji wa kadi za uanachama ingawa wanachama wengi wanaingia kwenye chama hicho hivyo ameshalifikisha kwenye uongozi wa juu na linashughulikiwa ikiwezekana uwepo wa mfumo wa kielektroniki.

“Wanachama wengi sasa wanahitaji kuja CCM lakini upatikanaji wa kadi zetu ni tatizo kwahiyo nitaliwasilisha kwa kinamna yake kwa mwenyekiti suala hili la kadi walipe kipaumbele ikiwezekana ziweze kupatikana kwa wakati”. Amesema

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar Salaam, Khadija Ally akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Adam Ngallawa amewasihi kamati ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kuhakikisha wanatumia michango kutekeleza miradi mbalimbali ili Juhudi za Jumuiya ya Wazazi zionekane na wanachama kuwa na imani na Chama hicho.

Washiriki katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

Amewataka viongozi wa kamati ya Utekelezaji kuwa kiungo kwa wazazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa wananchi wa mkoa huo kwani ndani yenu wamo vijana, wanawake,hivyo wametakiwa kuhakikisha Chama kinakuwa imara.

Washiriki wa mafunzo wakiwa makini kusikiliza.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally amesema watahakikisha wanahamasiisha ili ushindi wa kishindo unapatikana katika mkoa wa Dar es Salaam kwani wamejipanga kikamilifu kufanya vizuri kwenye kuelekea chaguzi zijazo.

Amesema kwa kuwa amechaguliwa kwa kuaminiwa hatahikikisha anatoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa chama hicho na ndo maana wakaona kuna umuhimu wa kupata mafunzo ya uongozi ili kila mmoja ajue mipaka yake.

Leave A Reply