Breaking News: Mwenyekiti Wa CCM Simiyu Afariki Dunia

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo amefariki dunia leo Februari 23, 2021 katika Hospitali ya Meatu mkoani humo.

 

Taarifa ya kifo hicho imethibitishwa na Katibu Mwenezi wa CCM, Mayunga George mkoani humo ambaye ameeleza kuwa taratibu za mazishi zitatolewa baadaye na familia ya marehemu.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amin.

Toa comment