The House of Favourite Newspapers

Mwenyekiti wa Chama Cha Mabenki Tanzania (TBA) Aongoza Maadhimisho Siku Ya Wanawake Duniani

0
Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi akitoa hotuba kwa washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake kutoka sekta za kibenki katika hafla iliyofanyika jana katika hoteli ya Onomo Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, Machi 16, 2023: Chama cha Mabenki Tanzania (TBA)  kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila Machi 8 kwa kusisitiza kuwa ni muhimu kwa taasisi zote za kifedha nchini kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii hususani wanawake ushirikishwaji wao unapewa kipaumbele.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Onomo  jijini Dar es Salaam mapema leo, Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi alisema ni muhimu sana kwa taasisi za kifedha kuhakikisha kunakuwa na ushirikishwaji mkubwa wa wanawake kwenye huduma za kibenki au kifedha nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA), Bi. Tusekelege Joune akitoa hotuba ya ufunguzi katika hafla hiyo.

“Tunatambua kuwa wanawake ni sehemu kubwa ya jamii yetu, zaidi ya asilimia 51 ya watanzania wote ni wanawake na kwa hivyo ni muhimu sana tunapoongeza ujumuishwaji wa kifedha kwenye jamii kundi la wanawake lisiachwe nyuma”. Alisema Sabi.

Bw. Sabi alibainisha kuwa kwa upande wa benki ya NBC wameanza na wafanyakazi wakijaribu kuhakikisha kuwa kama benki wanakuwa na sera rafiki kwa wanawake ili waweze kufikia malengo yao ya kikazi, kiajira, na kiuchumi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi akisaliamiana na Mkurungezi wa Benki ya Equity Tanzania Bi Isabela Maganga katika hafla hiyo.

Aidha naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA), Bi. Tusekelege Joune alisema kuwa inatia hamasa kuona kuwa benki nyingi nchini zimekuwa mstari wa mbele kubuni bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa maalum katika kukidhi mahitaji ya wanawake nchini.

Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika sekta za kibenki iliyofanyika katika Hotel ya Onomo Jijini Dar es salaam.

“Tunashukuru kuwa benki zimekuwa mstari wa mbele katika kuja na bidhaa mbali mbali ambazo zimekuwa mahsusi kwa ajili ya wanawake hapa Tanzania. iwe mwanamke mfanyabiashara, mwanamke mtanzania, mwanamke ambaye kwa namna moja au nyingine akihitaji huduma za kibenki anakutana na bidhaa ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake,” alisema Bi. Joune.

Bi Joune aliongeza kuwa maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani kwa upande wa sekta ya kibenki kumekua na ongezeko kwa  benki kuja na huduma ya dhamana maalum kwa ajili ya wanawake. Kutolewa kwa hati fungani kwa ajili ya maendeleo ya wanawake n.k ikiwa ni jitihada mbali mbali zinzofanywa na sekta hio katika kuinua jinsia ya kike.

Leave A Reply