The House of Favourite Newspapers

Mwezi Mtukufu… Mapenzi kaa mbali namii

0
Madee na Snura

NA ALLY KATALAMBULA | IJUMAA WIKIENDA

LEO ni siku ya tatu tangu kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo Waislamu wote ulimwenguni wapo katika ibada hiyo. Kutokana na hali hiyo, wapo baadhi ya Masupastaa wa Bongo ambao ni waumini wa dini ya Kislamu watakuwa pia wakitekeleza ibada hiyo.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kutekeleza, baadhi ya masupastaa hao wamekuwa wakiishi kinyumba na wanaume/ wanawake bila kufunga ndoa jambo ambalo ni kinyume na dini hususan katika kipindi hiki.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya masupastaa waliokuwa katika uhusiano bila ya kufunga ndoa wamefunguka kuhusiana na jinsi watakavyoweza kuishi katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.

Shilole na Wolper

SHILOLE

“Kwangu mimi hii ni zaidi ya ibada, sheria za kuishi na mume ziko wazi nitaingia kwenye mfungo kwa kufuata taratibu na sheria zote kama Mwenyezi Mungu alivyosema, mpenzi itabidi angoje hadi Ramadhani ipite.”

MADEE

“Mpenzi si kitu muhimu kama ibada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwangu mimi Ramadhani ni kitu kikubwa kuliko jambo lolote lile, nimekuwa nikifunga na kufanya ibada tangu nikiwa mdogo hadi sasa. Mpenzi na mambo mengine ya kijinga itabidi vingoje kwanza.”

SNURA

“Mpenzi si lolote wala chochote mbele ya Rehema za Mwenyezi Mungu, mpenzi wangu nimemweleza katika kipindi hiki lazima akae maili elfu moja kutoka mahali nilipo.”

Z Anto

“Ukijua thamani ya mwezi huu huwezi kukumbatia dhambi ya aina yoyote, nitalazimika kuwa mbali na mama watoto wangu hadi pale mwisho wa ibada hii.”

AMBER LULU

“Mimi siyo Muislamu lakini mpenzi wangu ni Muislamu, nitakuwa mbali naye ili nisimuharibie swaumu yake, katika kipindi hiki ambacho ni muhimu kwake, nilishasema na nitaendelea kusema mwezi huu Mtukufu nitasitisha kupiga picha nikiwa na vinguo vifupi.”

 

Stori zote kali za leo tembelea ukurasa wa facebook wa Gazeti la Ijumaa Wikienda ===>https://www.facebook.com/IjumaaWikienda/

Leave A Reply