The House of Favourite Newspapers

Soma Hapa… Makadirio Na Matumizi Ya Bajeti Kuu 2024/2025 – Video

0
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Serikali imesema bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 imelenga kutekeleza vipaumbele vitakavyojikita katika kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu” pamoja na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2024/25.

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni Dodoma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba  Juni 13, 2024 ameyataja maeneo ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango huo kuwa ni pamoja na kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, kukuza biashara na uwekezaji, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu.

“Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliyopo sasa hadi asilimia 40. Vilevile, Mheshimiwa Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33, sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa fedha huu.”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha bungeni Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/24. Ameongeza, “Serikali itaendelea kuangalia maslahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko.” SOMA HAPA CHINI

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU (MB),
AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2024/25

 

Leave A Reply