The House of Favourite Newspapers

Mwigulu Asimulia Punda Walivyotaka Kumtoa Uhai Leo – Video

  MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, ambaye amepata ajali ya gari ilitokea leo Jumatano Februari 13, katika eneo la Migori Mkoani Iringa akiwa safarini kuelekea Singida kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa, amesema chanzo cha ajali aliyopata ni dereva kukwepa punda watatu.

 

“Wakati tukiendelea na safari, ghafla walikatisha punda nadhani walikuwa watatu, dereva wangu alitoa ishara kuwa kuna kitu cha hatari, ilikuwa ni kitendo cha kufungua macho tu tayari tukawa tumeshagongana.

“Nilisikia kishindo kikubwa na moshi litanda ndani ya gari, ilikuwa imepinduka. Wasamaria wema wakaja kutuchukua na kutuleta hapa hospitalini, lakini namshukuru Mungu kutoka mzima kwani mkanda ulikuwa umenibana sana, mwanzo nilijiona kama sijaumia lakini baadaye nilisikia maumivu kwenye kifua na kiuno,” amesema.

 

Mwigulu amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma akiendelea na matibabu na amesema kwa sasa anaendelea vizuri.

 

MSIKIE MWIGULU AKIZUNGUMZA

Comments are closed.