The House of Favourite Newspapers

Mwigulu awatimua Kazi Viongozi Matapeli wa Vyama vya Tumbaku-Iringa

1
Mwigulu (1) Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba akisalimiana na wadau wakati wa mkutano wake na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika pamoja na wakulima, Iringa.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba amewasimamisha kazi viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku mkoani Iringa wanaotuhumiwa kushiriki katika ufisadi wa mkopo wa matrekta 9 kupitia mgongo wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku na kujimilikisha wenyewe.
Mwigulu (2)
Mwigulu akisalimiana na wadau
Nchemba alifikia hatua hiyo jana baada ya wakulima wa tumbaku kuwalalamikia viongozi wa vyama hivyo kwa kuwatapeli.
Mwigulu (3)
Wakulima wa tumbaku wakiwasilisha malalamiko yao kwa Waziri Mwigulu Nchemba.

Matrekta hayo 9 yaliyoleta mzozo vilikopeshwa vyama vya Msingi  na benki ya CRDB kwa manufaa ya wote na wakulima wamekuwa wakitozwa pesa wanapoyatumia matrekta hayo ili kulipia madeni benki.

Katika utetezi wao, viongozi  hao wa vyama walimwambia Waziri kuwa Matrekta hayo siyo ya vyama bali ni ya kwao ila walikopa kupitia mgongo wa Vyama vya msingi vya ushirika.

Mwigulu (4)Mkutano ukiendelea.

Waziri Nchemba aliwahoji viongozi hao kama kuna kiongozi  aliyelipia mkopo wa  matrekta hayo kwa fedha yake ambapo  wote walisema hawajalipia ila wamelipiwa na wanachama lakini walipanga yatakuwa ya kwao kwa kuwa wao ndio wanaosimamia ukusanyaji wa fedha za wanachama kuyalipia Matrekta hayo.

Utetezi huo ulimtia kichefuchefu Waziri Nchemba  na kuamua kuwafukuza kazi viongozi hao na kuamuru benki ya CRDB waandike kadi za matrekta hayo kwa umiliki wa vyama vya Msingi.

1 Comment
  1. Urio says

    Hiyo ndiyo kazi ambayo inahitajika kwa kila mtendaji wa serikali ili kuondoa kufanya kazi kwa mazoe na kwa njia ya madili ili kujinufaisha wachache. Hongera sana Mh. Waziri!

Leave A Reply