Mwijaku Amuomba Radhi Mtangazaji Mwenziye Masoud Kipanya – Video
Mtangazaji na muamasishaji wa mambo mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii Burtoin Mwenda ‘Mwijaku’ amemuomba radhi Mtangazaji mwenziye Masoud Kipanya kwa kile alichokiongea siku za hivi karibuni.
Mwijaku baada ya kuondoka Clouds Media na kuhamia Crown Media, Masoud Kipanya alitoa maoni yake ambayo yalionekana kumkera Mwijaku.
Baada ya Masoud kuongea Mwijaku aliandika ujumbe mbaya mitandaoni kuhusu Masoud Kipanya.
Mapema leo hii mbele ya waandishi wa habari ametumia fursa hiyo kumuomba Radhi @masoudkipanya na kusisitiza kuwa ni mtu ambaye anamuheshimu sana na ataendelea kumuheshimu sana.